Taarifa kwa Umma Kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Madini

Mabadiliko ya sera za kiuchumi yaliyofanyika miaka ya 1990 na Sera ya Madini ya mwaka 1997 yaliweka vivutio vya uwekezaji kwenye sekta ya madini na kuharakisha ukuaji wake. Matokeo ya uwekezaji huo ni kuanzishwa kwa migodi mikubwa saba ya dhahabu iliyoanzishwa kati ya mwaka 1998 na 2010. Migodi hiyo ni: Golden Pride uliopo Nzega, Geita uliopo Geita, Bulyanhulu uliopo Kahama, North Mara uliopo Tarime, Buhemba uliopo Musoma Vijijini, Tulawaka uliopo Biharamulo, na Buzwagi uliopo Kahama.

Attachment: attachment TAARIFA_KWA_UMMA_KUHUSU_MAENDELEO_YA_SEKTA_YA_MADINI
© 2018 Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) All Rights Reserved.