Mchango na Manufaa ya Sekta ya Madini katika Uchumi wa Tanzania

Mabadiliko ya sera za kiuchumi yaliyofanyika miaka ya 1990 na Sera ya Madini ya mwaka 1997 yaliweka vivutio vya uwekezaji kwenye sekta ya madini na kuharakisha ukuaji wake.
Matokeo ya uwekezaji huo ni kuanzishwa kwa migodi saba mikubwa ya dhahabu iliyoanzishwa kati ya mwaka 1998 na 2009. Migodi hiyo ni:

- Golden Pride uliopo Nzega,
- Geita uliopo Geita,
- Bulyanhulu uliopo Kahama,
- North Mara uliopo Tarime,
- Buhemba uliopo Musoma Vijijini,
- Tulawaka uliopo Biharamulo, na
- Buzwagi uliopo Kahama.

Attachment: attachment Mchango_na_Manufaa_ya_Sekta_ya_Madini_ktK_Uchumi
© 2018 Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) All Rights Reserved.